Search This Blog

Wednesday, April 1, 2015

Tuko kwenye mwaka wa uchaguzi, tuwe makini na watu wanao taka uongozi kwa nguvu nyingi, tukumbuke ikulu sio mahali pa kukimbilia. tuchague viongozi wenye nia ya dhati ya kuleta maendeleo na sio wanaotaka kunenepesha matumbo yao.

chagua mgombea umtakae bila shinikizo la mtu yeyote, pia katika katiba mpya tuisome, tuielewe na kisha tufanye maamuzi sahii kwa kupiga kura ya ndio au hapana kutegemeana na ulivyo ielewa.

Tanzania na nchi zingine nyingi duniani zinakabiliwa na janga la ukosefu wa ajira, vijana wengi wanao maliza vyuo vikuu na vyuo vingine, wapo mtaani hawajui ch kufanya kutokana na upungufu wa ajira kataka nchi zao. lakini wewe kama kijana mwenye akili timamu na nguvu hupaswi kuzurura mtaani kutafuta ajira, badala yake ingia kwenye ujasiriamali na utafanikiwa sana kiuchumi na pia unaweza hata ukaajiri. katika nchi yetu fursa ni nyingi sana ambazo zikitumiwa vizuri zitaleta maendeleo ya mtu binafsi lakini pia kwa taifa zima.
vijana tutafute fursa za ujasiriamali tufanye kazi tuache uvivu wa mwili na wa akili ili tukaribiane na tatizo la ajira.www.facebook.com